Kala Pina: Makonda Tobo la Unga hili Hapa!

 Sakata la mastaa na watu mbalimbali wanaohusishwa katika matumizi pamoja na biashara ya kuuza na kutumia madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kupamba moto na kuchukua sura mpya kila siku kwenye media na mitandao mbalimbali ya kijamii.

Vita ndiyo kwanza imeanza, ambapo mwanamuziki ambaye pia ni mwanaharakati anayepambana kuhakikisha vijana wanaacha kujihusisha na madawa hayo Bongo, Kala Pina anafunguka mtazamo wake katika vita hii, nini kifanyike ili kuhakikisha suala la madawa ya kulevya  linakuwa historia Bongo.

Kupitia showbiz, aliyokuwa akihojiwa Kala Pina, Moja ya maswali aliyoweza kuulizwa Kalapina ni..  

Mpaka hapa sakata hili lilipofikia kipi unaweza kumshauri Makonda? Kala Pina alijibu.. "Atushirikishe wadau ambao tupo kwenye vita hii kwa muda mrefu, tuna mambo mengi mno ambayo yanaweza kusaidia katika kuimaliza vita hii kwani tunaelewa tobo la biashara hiyo lilipo.

Swali lingine lilikuwa.. Unamaanisha nini unapozungumzia tobo la biashara ya unga? Kala Pina alijibu... "Namaanisha watafutwe wafanyabiashara wakubwa wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, mabig don au papa. Nazungumzia wanaoingiza madawa hapa nchini. Kikubwa wanajulikana na siyo suala la siri, hata njia zao zinajulikana, wanaingiza kupitia baharini. Sasa huko kukidhibitiwa hawa vijana wengine namaanisha wasanii wenzangu waliokamatwa wenyewe wasaidiwe kujinasua huko kwenye matumizi.

 

Powered by Blogger.