JK kumtia kitanzini Nikki Mbishi? Aitwa Basata
Msanii Nikki Mbishi ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'I'm sorry JK', huenda akaingia matatani baada ya kutakiwa kuripoti katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu ujumbe uliomo kwenye wimbo huo.
Katika wimbo huo Nikki anaonesha
kumuomba radhi aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete huku
akidai kuwa Watanzania hadi sasa tayari wameshamkumbuka Rais huyo
mstaafu kutokana na namna alivyokuwa akiongoza nchi, akifananisha na
namna ambavyo uongozi mpya umekuwa ukiendesha nchi.
Nikki ndani ya ngoma hiyo kuna
mstari anasema "Mikopo hakuna tena na wala chuoni watu hawaendi
kizembe", ukiwa ni mstari mmoja kati ya mistari kadhaa ambazo huenda
zikawa ndiyo sababu ya BASATA kuhitaji maelezo ya kujirishisha kutoka
kwake kiasi cha kumuomba afike ofisini ili kujadili mustakabali wa wimbo
huo.
Kwa upande wake Nikki Mbishi amesema
amechelewa kupata ujumbe huo wa BASATA kutokana na matatizo ya msiba
hivyo alishindwa kufika kwa muda ambao ulikuwa umepangwa ila anasema kwa
kuwa aliitwa atafika BASATA na kujadili nao.
"Leo (jana) tarehe
13/02/2017 nimehitajika kuripoti ofisi za BASATA ambapo wanadai
walinitumia ujumbe zaidi ya siku 3 nyuma ila sikuwa hewani labda kwa
sababu ya msiba ulionipata, kufuatia ujumbe niliyotumiwa juzi tarehe
09/02/2017 kwa njia ya message za kawaida za simu ya kiganjani". Amesema
Nikki
Akiutaja ujumbe huo, Nikki amesema ujumbe ulikuwa unasema "Habari za jioni? Tafadhali fika bila kukosa BASATA kesho 10/02/2017 saa tatu kuzungumzia mustakabali wa wimbo wako wa " I AM SORRY JK" aliandika Niki Mbishi