Je The Amazing inaongeza idadi ya members? Hili hapa jibu la Izzo Bizness


Miongoni mwa makundi yanayotawala anga la Bongo kwa sasa, ni kundi la The Amazing linaloundwa na wakali Izzo Bizness pamoja na Abela Music. 

Kundi hilo limejizolea umaarufu mkubwa kwa kipindi kifupi kutokana na kazi zao, umaarufu ambao umefanya wafuatiliwe zaidi na mashabiki ambao wanatamani kufahamu vitu vingi kutoka kwao.

Miongoni mwa vitu ambavyo mashabiki wanatamani kufahamu kutoka kwa The Amazing, Ni je kundi hilo litaongeza idadi ya members kwenye kwepo kwenye kundi hilo? Swali ambalo limejibiwa na Izzo Bizness.

“Kwa saa hizi bado ni mapema,kwasababu kundi lenyewe tunapambana kulisimamisha kwa level za juu zaidi..kuna miziki mingi tunarekodi,so tunasubiri kuwaaminisha watu kwa kile ambacho tunafanya,” Izzo ameiambia Dizzim Online.

Mpaka sasa kundi hilo limeshafanya kazi na producers Abbah na Duppy japo Izzo amedai kuwa wao wapo tayari kufanya kazi na producer yoyote japo ngoma yao ijayo imefanywa pia na Abbah.
Powered by Blogger.