Imethibitishwa! Wema Sepetu Kahamia Chadema Na Hii Ndio Kauli Yake Yake Ya Kwanza Baada Ya Kurudisha Kadi Ya CCM


Wema Abraham Isaac Sepetu, Tanzanian Sweetheart, Beautiful Onyinye ama Kipenzi cha watanzania amethibitisha kujiunga rasmi na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kitu ambacho kisingeweza kufikirika kwa haraka kufuatia nguvu ambayo mrembo Wema aliionyesha kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015 alipokipigia debe Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 Sasa katika kuwatoa wasiwasi waliodhani mmrembo huyo amepewa pesa na uongozi wa CHADEMA, mpiga picha wa Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa twitter @Besttizo ameandika ujumbe ulionukuliwa kutoka kwenye kauli za Wema ukionyesha waziwazi mrembo huyo na mama yake wamhamia  chama hicho kwa mapenzi yao na sio ushawishi wa mtu yeyote.

Powered by Blogger.