Ikiwa Vannesa Mdee Naye Anahitajika Kituoni, Wema Sepetu Na Wengine Bado Waendelea Kushikiliwa Na Polisi


Ni jana ndio ilikuwa siku ya kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda, kwa wasanii na watu wengine maarufu, Ambao Mh aliwataka kufika kituo kikuu siku ya jana bila kukosa juu ya mambo yote yanahusisha tuhuma za madawa ya kulevya.

Wema Sepetu, Tid, Nyandu Tozi, na Babuu ni baadhi ya wachache ambao  waliitikia wito wa Mh Paul Makonda.

Vanessa Mdee

Na katika wasanii wote ambao walifika kuitikia wito huo wa Mh Makonda wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi. Kamanda wa polisi Kanda maalum Dar Es Salaam Simon Sirro amethibitisha hilo.

Lakini pia msanii Vannesa Mdee ametakiwa kufika bila kukosa siku ya jumatatu ya tarehe 6/2/2017, pamoja na video queen Tunda.
Powered by Blogger.