HEE! KUMBE BADO YUMO HUYU JAMAA


Aliyekuwa Golikipa wa vilabu vya Simba na Yanga Mbeya city na timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Starz"  ang'ara ligi kuu ya Vodacom 2016/2017.


Golikipa huyo ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera mjini Bukoba amepewa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari katika ligi kuu ya Vodacom mwaka 2016/2017.
Katika tuzo hiyo walikua wanachuana na mchezaji mwenzake wa Kagera Sugar Mbaraka Abeid na mchezaji wa Jamal Mtengeta wa klabu ya Toto Africans ya Mwanza.
Na Tuzo hiyo kunyakuliwa na Juma Kaseja kwa Vigezo vyake na kwa Takwimu za mwezi Januari ya kufungwa goli moja katika mechi tatu za ligi kuu mwezi Januari na klabu yake kufunga magoli sita.
Kwahiyo mshindi huyo anapewa kitita cha Tsh, milioni moja za Kitanzania.


Powered by Blogger.