Hatimae Manji apata dhamana hii juu ya Shitaka la kutumia dawa za kulevya

 
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10. Manji alipandishwa kizimbani leo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka la kutumia dawa za kulevya.

Manji amedhaminiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa. Kabla ya hapo mfanyabiashara huyo alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya moyo yaliyompata baada ya kushikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi Central.

Kwenye kesi hiyo Manji anashutumiwa kutumia dawa za kulevya aina ya heroin kutokana na vipimo toka kwa Mkemia Mkuu wa serikali. Mshtakiwa amekana kosa hilo.
Powered by Blogger.