Harmorapa 'Talk of the town', Vipi Angekuwa Hitmaker?Harmorapa ametrend mtandaoni kwa mwezi mfululizo sasa, yani kwa publicity anayoipata ni kubwa sana.

Nini hasa kinachomfanya atrend na awe kwenye midomo ya watu? Muziki wake? Hapana, I bet asilimia 80 ya watu wanaomshangilia hawajui hata wimbo wake unafananaje, sababu hadi sasa video yake ingekuwa na zaidi ya views milioni 1. Kwahiyo, nini hasa story yake? Kwanini anaongelewa sana?

Well, ni ile wazungu wanaiita ‘public ridicule’, ama ‘mzaha wa umma.’ Umaarufu wake umezungukwa na dhihaka na utani mwingi. Iko hivi, Harmorapa ameanza kufahamika baada ya kuibuka na kudai kuwa anafanana na Harmonize, na wengine wakaanzisha mzaha kuwa ni ndugu yake.

Na hata jina lake lina maana ya kuwa yeye ni Harmonize anayerap. Kwa muda mfupi watu wakaanza kumfuatilia na kwakuwa binadamu hupenda vitu kama hivi – mzaha, jina lake likasambaa haraka na focus ikahamia kwake, kuliko hata Harmonize mwenyewe. Naamini hadi sasa wapo watu wanaomfahamu zaidi yeye kuliko hata Harmonize.

Harmorapa, ama mtu aliye nyuma yake akawa smart kiasi. Akaja na mwanamke ambaye naye akatambulishwa kama version yake ya Wolper, ex wa Harmonize.

 

 Harmorapa sasa naye ana Wolper wake. Amekuja kupata kiki zaidi baada ya dancer wa Diamond, Mose Iyobo kumfananisha na nyani. Hapo, akaanza kupokea ‘public sympathy’ (huruma ya umma), ambayo inazidi kumpaisha zaidi. Yuko smart naye, ameitumia hiyo kujikusanyia huruma kutoka wa watu wengi ambao ajabu ni kuwa wengi hawajui hata wimbo wake, they don’t care actually.

Kwao, Harmorapa ni mtu anayewachekesha, well kwa namna alivyoibuka kwanza na sura yake ilivyo. Hivi karibuni alionekana kwenye picha akiwa ameshikilia malundo makubwa ya fedha na picha ikasambaa kwa kasi mtandaoni hadi kumfikia producer, P-Funk Majani.

“Chezea @harmorappa wewe!!! Levo zingine hizi,” aliandika Majani kwenye picha hiyo na kuchomeka emoji ya kicheko. Hakuna ubishi, Harmorapa ametokea kuwa burudani kwa wengi.

Swali langu ni kuwa, vipi kama Harmorapa angekuwa na kipaji kweli cha kurap au kuimba, kwa publicity hii anayopata, unadhani ingekuaje? Sababu kiukweli, hakuna anayechukulia serious muziki wake, lakini publicity anayoipata, kuna wasanii wakubwa hawajahi kuipata tangu waanze muziki.

Ninachoomaanisha ni kuwa, kama angekuwa na muziki mzuri mkononi mwake, dogo angekuwa keshatusua na kila siku angekuwa busy na show. Napenda attitude yake lakini, ya kujiamini hadi kusema kuwa level zake ni sawa na za akina Fid Q!
Powered by Blogger.