Country boy adai sakata la madawa ya kulevya lachelewesha kutoka kwa video yake mpya

 

Tangu wiki iliyopita, story kubwa Tanzania imekuwa ni sakata la vita ya madawa ya kulevya ndani ya Dar es Salaam inayoendeshwa na mkuu wake wa mkoa, Paul Makonda.

Huenda sakata hili likawa limeathiri shughuli nyingi za kisaana ikiwemo kutoka wa video ya wimbo wa Hakuna Matata wa Country Boy.

Msanii huyo ambae yupo chini la Label ya L.F.L.G alitoa ahadi ya kuachia video hiyo wiki hii, lakini haijatoka na kupitia kipindi cha Supermega cha Kings Fm, rapper huyo amekiri kuwa kuna vitu vilikwama kwani mabosi zake (Petit Man na Mchafu Chakoma) walikua miongoni mwa watu waliokamatwa kwenye sakata hilo.

“Ilikua tayari tushapanga mipango lakini haikukatisha kabisa kwamba tushindwe kufanya video. Tayari program zingine zilikuwa zinaendelea, Hiyo pia ilikuwa moja ya sababu kwasababu ndio watu ambao walitakiwa wafuatilie vitu moja kwa moja,” amesema Country Boy.

Pia amedai kuwa mwishoni mwa wiki hii video hiyo itakuwa tayari na muda wote itaanza kuonekana kwenye vituo vya runinga na mtandaoni.
Powered by Blogger.