CAMEROON MABINGWA AFCON 2017

Hatimae Timu ya Taifa ya cameroon yatwaa ubingwa wa Africa yaani AFCON 2017 kwa kuwachapa mafarao wa Misri kwa goli 2-1 katika mchezo huo uliofanyika katika dimba Stade de Angondje nchini Gabon.
Mtanange ulianza kwa misri kujipatia goli la kwanza kupitia kwa kiungo wake anayeichezea klabu ya Arsenal Mohamed Elneny dakika ya 22 nakuelekea kwenye mapumziko wakiwa wanaongoza kurudi kwenye kipindi cha pili dakika 58 cameroon walisawazisha kupitia kwa beki wake Nicolas N"Koulou na mchezo huo kumaliziwa na mshambuliaji wa cameroon Vincent Aboubakar katika dakika ya 88 kuiandika goli la pili na la ushindi huo.

Cameroon inafikisha makombe matano kwa sasa baada ya kuchukua hili.
Powered by Blogger.