Bondia Mohammed matumla atakua nje ya ulingo kwa mwaka mmoja.


Bondia mohammed rashid matumla atakua nje ya ulingo kwa mwaka mmoja kwa mujibu wa daktari.

Daktari wa hospitali ya Taifa muhimbili kitengo cha upasuaji Othman kiloloma ameeleza kuwa bondia huyo kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji katika eneo la kichwa katika sehemu ambayo imeathirika kwa damu kuvilia kwenye ubongo kitaalam ni (Acute Subdyral Hemotema) iliyotokana na mgandamizo.

Baada ya kupigwa konde kali na mwanamasumbwi mwenzake Mfaume mfaume katika pambano hilo lisilo na ubigwa lililopelekea kijana huyo wa mwanamasumbwi wa zamani Rashidi matumla kuumizwa maeneo ya kichwa nakumpelekea kuanguka chini katika mzunguko wa saba na kupelekea kukimbizwa hospitali..
kwa hiyo bondia huyo kwa sasa anapatiwa matibabu ambayo yatamfanya arudi katika hali yake ya kawaida ambayo itamchukua miezi 8 hadi 12 ili aweze kuwa mzima na kurejea kwenye ulingo.alisema daktari huyo 

Powered by Blogger.