#TBT Nyimbo 10 Zilizofanya Vizuri Kwenye Chati Ya Billboard Top 100 Mwezi Februari Mwaka 2016


Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard hizi ni nyimbo 10 miongoni mwa nyimbo 100 ambazo zilifanikiwa kufanya vizuri katika kipindi cha mwezi Februari mwaka 2016.

1: Justin Bieber - Love Your Self:

Justin Bieber alishikiria rekodi hii kwa zaidi ya mwezi mzima na wimbo wake "Love Yourself" ambao umekaa kwenye Chati kwa zaidi ya wiki 13 huku video yake ikiangaliwa zaidi ya mara Bilioni 1 kwenye mtandao wa Youtube.

 2:twenty one pilots: Stressed Out Kutoka kwenye Albamu "Blurryface" kundi la Twenty One Pilots waliingiza ngoma yao "Stressed Out" ambayo imekaa kwenye chati hizo zaidi ya wiki 21 kwenye mtandao wa youtube Video ya wimbo huo imeangaliwa zaidi ya mara milioni 800. 


3: Justin Bieber - Sorry Kutoka kwenye Albamu yake "Purpose" Justin Bieber aliingiza hitsong sorry ambayo ilikaa kwenye chati hizi kwa wiki 16 na kumfanya kuwa msanii mwenye ngoma zaidi ya moja kwenye zile kumi kali kwa wiki hiyo. Video ya wimbo huo ambayo inawaonyesha watoto wa kike wakicheza mwanzo mwisho ndio video ya Bieber inayoongoza zaidi kwa kuangaliwa kuliko video zake nyingine, imeangaliwa zaidi ya mara bilioni 2. 

 4:Rihanna - Work Feat. Drake Licha ya kupigwa kwenye Tv, Radio, Night Clubs na maeneo mbalimbali ya kiburudani Work ya Bad Girl RiRi na mnyamwezi Drake nayo iliweza kuzipamba chati hizi kwa zaidi ya wiki 3, Kwenye mtandao wa Youtube video hii imetazamwa zaidi ya mara milioni 800' 

5: FloRida - My House Florida alizishikiria chati za Billboard kwa wiki 14 huku video yake "My House" ikiangaliwa zaidi ya mara milioni 100 kwenye mtandao wa youtube. 

 6: Adele - Hello Kwa wiki 16 Hello ya Adele ilimiliki namba kadhaa kwenye chati hizi huku video yake ikitazamwa zaidi ya mara bilioni 1.8. 

7: Zayn Malik - Pillow Talk Albamu yake 'Mind Of Mine' ilimuweka Zayn kwenye headlines hususan ngoma hii Pillow Talk ambayo ilifanikiwa kukaa kwenye chati hizi kwa wiki mbili 2, Kwenye mtandao wa youtube Video ya wimbo huu imneangaliwa zaidi ya mara milioni 800. 

8: G-Eazy x Bebe Rexha - Me, Myself & I Kwa zaidi ya wiki 15 G-EAZY aliingiza ngoma yake "Me,Myself n I" kwenye chati za Bilboard huku kwa upande wa youtube video hiyo ikitazamwa zaidi ya mara milioni 250. 

 9:Roses The Chainsmokers Featuring Rozes: Huku ikiwa na views zaidi ya milioni 111 "Roses" ilifanikiwa kukaa kwenye chati hizi kwa zaidi ya wiki 17. 

 10: 
Stitches - Shawn Mendes
Powered by Blogger.