Bayern yaibebesha Arsenal 5, wazidi kuendeleza rekodi yao mbovu

Usiku wa February 16 2017 michezo ya hatua ya 16 bora ya michuano ya Club Bingwa Ulaya ilichezwa katika viwanja viwili barani Ulaya, wakati Real Madrid alikuwa mwenyeji wa Napoli, timu ya Arsenal ilisafiri kutoka London hadi Munich Ujerumani kucheza dhidi ya FC Bayern Munich.

Arsenal ambao walikuwa wakiingia katika mchezo huo wakiwa na rekodi ya kucheza na FC Bayern Munich mara nne katika miaka mitano iliyopita katika hatua ya mtoano, wamekumbana na kipigo cha goli 5-1, kabla ya game hiyo kuanza rekodi ilikuwa inaiua Arsenal kwani toka 2012 hajawahi kuvunga mchezo wake wa kwanza wa hatua ya mtoano, michezo yote amekuwa akipoteza.

FC Bayern Munich walianza kuiadhibu Arsenal dakika ya 11 Arjen Robben lakini Arsenal walisawazisha goli hilo dakika ya 30 baada ya Sanchez kupiga penati kukosa halafu akamalizia, kipindi cha pili Robert Lewandowski dakika ya 53 ndio alianza kuizamisha Arsenal baada ya kufunga goli la pili.

Kiungo Thiago Alcantara akapachika magoli mawili dakika ya 56 na 63 lakini Thomas Muller akaja kuhitimisha idadi ya magoli la kufunga goli la 5 liliimaliza Arsenal, kipigo hicho kinakatisha tamaa Arsenal licha ya kuwa bado wanamchezo mmoja nyumbani lakini kuifunga Bayern zaidi ya goli nne inaonekana kama mtihani.
Powered by Blogger.