Barcelona yatinga fainali ya copa del rey


Barcelona waweka rekodi kwa mara nyingine kwa kutinga fainali za copa del rey nchini hispania kwa kuwatoa atletico madrid.

katika mchezo huo uliochezwa usiku wa kuamkia leo hii katika dimba la barcelona Nou camp na kuwaalika wageni wao atletico de madrid katika mchezo huo uliotawaliwa na soka safi kutoka kwa timu zote hizo mbili  pamoja na kutoka kadi za kutosha.Barcelona walianza kwa mchezo wao wa pasi ambapo walishindwa kuwapita wachezaji wa Diego Simeone kwenye lango lao hadi pale mshambuliaji wa barcelona alipopiga mpira mkali ambapo kipa wa atletico madrid aliupangua na kumkuta luis suarez na kushinda goli la kwanza dakaka ya 42 kipindi cha kwanza.

katika kurudi kipindi cha pili katika dakika ya 79 atletico de madrid walipatiwa penati baada ya mchezaji wake Kevin Gameiro kufanyiwa madhambi ndani ya box nakupiga penati hiyo ambayo alikosa kwa kupaisha juu ya lango la wapinzani ndipo dakika ya 82 Antonie Griezmann kutoa pasi ya goli kwa mchezaji mwenzake Kevin Gameiro lililosawazisha goli la Barcelona.
Nako dakika ya 89 Luis Suarez alicheza rafu iliyompelekea apewe kadi nyekundu ambapo itamkosesha mechi ya fainali akiwa anaitumikia adhabu hiyo hadi mchezo unamalizika kwa sare pacha hiyo atletico de madrid anakuwa hana nafasi ya kusonga mbele.
Kwa matokeo hayo Barcelona inakuwa imeshinda ushindi wa jumla kwa goli 3-2 nakuwapeleka fainali.
Powered by Blogger.