AZAM YAWAADHIBU WAGENI WAO WA ZAMBIA

Klabu ya Azam ya jijini Dar es Salaam yawaadhibu wageni wao kutoka nchini Zambia Red Arrows.

Klabu ya Azam jana usiku ilikua na mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Red Arrows kutoka nchini Zambia. Katika mchezo huo uliochezeka katika uwanja wa Azam Complex  Mbagala Chamanzi na Azam kujipatia ushindi wa goli moja kwa bila kutoka kwa beki wake Abdallah Kheri ambaye kwa siku ya jana alicheza nafasi ya kiungo mkabaji baada ya kupigwa mpira wa adhabu ndogo na mchezaji mwenzake wa Azam Khamis Mcha na yeye kuuzamisha kwenye nyavu za Red Arrows dakika ya 84 na  kuiandikia timu yake goli.
Azam ilivitumia vikosi vyake vyote viwili katika mchezo huo na pia kwa mara ya kwanza Kocha wao kukaa katika benchi la ufundi baada ya kukamilisha vibali vya kufanya kazi nchini.
Naikumbukwe kuwa Azam wana michuano ya Kimataifa ya Shirikisho wanayotarajia kuanza kushiriki.

Powered by Blogger.