AZAM KUKIPIGA LEO USIKU NA ZAMBIA


Klabu ya Azam leo ina mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Red Arrows ya nchini Zambia katika uwanja wa azam complex chamazi jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kujipima kwa timu zote mbili kwa azam unakuwa mchezo wake wa pili wa kujipima baada ya kucheza na mabingwa wa Afrika Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika Kusini na  kutoka nao sare pacha ya bila kufungana.
 Kwahiyo mchezo wa leo unakuwa ni mchezo wa pili wa kujipima kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika iliyo mbele yao.Pia kwa upande wa Red Arrow unakuwa ni mchezo wao wa kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya nchini kwao Zambia.

Pia kwa upande wa wageni hao waliotuwa nchini Tanzania mwanzoni mwa wiki wamewamwagia sifa kemkem wenyeji wao kwa kuwa na miundombinu bora na iliyojitosheleza na kusema kuwa Sisi tuko hapa kwa ajili ya kujijenga, unajua Azam FC ni klabu bora na yenye ujuzi, ni klabu iliyoko kwenye michuano ya Afrika, tumeiona ni timu iliyojipanga, inaonekana ipo na ujuzi zaidi, wamejipanga kuanzia kwenye uongozi, programu za kila siku na mazoezi, sisi tunajisikia furaha kujihusisha na klabu kama hii na sisi tunataka kuingia kwenye njia kama ya kwao.
Wameichagua klabu hiyo kwa ajili ya kupata changamoto kutoka katika klabu hiyo ya Azam kwa sababu wao wanashiriki mashindano ya kimataifa na pia kushukuru kwa mapokezi yao.alisema kocha wao Honor Janza ambaye alikuwa ni kocha wa timu ya Taifa ya Zambia "chipolopolo". 

Timu hiyo imeshachukua kombe la ligi ya Zambia mwaka 2004.
Powered by Blogger.