ASAMOAH AFUNDISHWA NIDHAMU YA NYWELE UARABUNI

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Ghana Asamoah Gyan amepewa somo la nidhamu ya nywele nchini Uarabuni.

Mchezaji huyo wa klabu ya Shangai  SIPG ya nchini China amepata majanga hayo baada ya  kutolewa kwa mkopo katika klabu ya Al Ahli ya falme za kiarabu nchini Dubai amepewa likizo ya kutokucheza mchezo wa mpira hadi hapo atakaponyoa au kuondoa nywele alizoziacha katika kichwa chake hicho mtindo wa "denge" ambao amekuwa akiutumia mara kwa mara katika kunyoa.
Asamoah Gyan sio wa kwanza kukutana na adhabu hiyo ishawi kumtokea mchezaji Waleed Abdullah aliyekua anacheza nafasi ya golikipa katika moja ya klabu ya nchini humo. 
Hiyo inatokana na sheria za maadili za nchi hizo za kiaarabu.


Powered by Blogger.