Ali Kiba Awasili na Tuzo ya MTV Kutoka Sauzi, Apokelewa na NyomI


MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Ali Kiba amewasili mchana huu akitokea nchini Afrika Kusini, alikoenda kukabidhiwa tuzo yake ambayo alishinda lakini yakafanyika magumashi na kupewa msanii mwingine.
Baada ya akuwasili uwanjani hapo, Ali Kiba alipokelewa na nyomi ya mashabiki wake waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, ambapo alipata nafasi ya kuzungumza machache kabla ya kuingia kwenye gari maalum lililokuwa limeandaliwa, kisha kuondoka huku akisindikizwa na mashabiki wake.
kabla ya kukabidhiwa tuzo hiyo ya MTV, licha ya kushinda, alitangazwa msanii mwingine, Wiz Kid kwamba ndiye aliyeshinda lakini baada ya menejimenti ya msanii huyo kusimama kidete, baadaye MTV wakakiri kwamba mshindi halali alikuwa ni Ali Kiba na kuahidi kumpa tuzo yake, jambo ambalo hatimaye limetimia.

Powered by Blogger.