Kingine Unachotakiwa Kujua Kuhusu Harrysongz Na Five Star Music

Kama ni mfuatiliaji wa mastori ya Nigeria utakua uliwahi kukutana na ishu iliyomuhusisha  hitmaker wa "Reggae Blues" ushaelewa kama hapa namuongelea HarrySongz ambae mwishoni mwa mwaka wa jana alitangaza kuachana na uongozi wake yaani "Five Star Music" ya Nigeria inayoongozwa na ndugu E-Money pamoja na KCEE.Baada ya kuipiga chini Five Star  mnyamwezi Harrysongz alienda kuanzisha Record Label yake mwenyewe iliyojulikana kama "ALTERPLATE”.

Uongozi wa  Fivestar Music haukuipotezea ishu hiyo  ilihali walikua bado wana haki ya kuwa na Harrysongz kwenye timu yao, hivyo waliamua kudai haki zao ikiwemo faini kwa Harrysongz ambae aliamua kuondoka kabla ya mkataba wake kuisha, Ishu ilizidi kuwa kubwa mpaka wakafikia pointi ya kupelekana polisi.

Goodnews ni kwamba Five Star na Harrysongz hawana beef tena na tayari mshikaji amerudi kundini.


"I miss my family, Love forever @fiverstarmusicng" .Ameandika Harrysongz kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Powered by Blogger.