Yemi Alade Apata Mwaliko Wa Kuhudhuria Kwenye Tuzo Za Grammy 2017


Afrika inazidi kusonga mbele na kufanya vizuri kwenye sekta ya muziki kwa kuwakilishwa na wasanii kibao kutoka kila pande ya Afrika, Sasa msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade anaye tamba na kibao chake cha “TumBum”, ameamua kushare na sisi jambo hili.

Nyota wa muziki nchini Nigeria, Yemi Alade, ametumiwa mwaliko wa kuhudhuria katika tamasha la utoaji tuzo za ‘Annual Grammy Awards’ ambazo zitatolewa Februari 12, mwaka huu.

 View image on Twitter

Tuzo hizo za 59, zitatolewa kwenye ukumbi wa Staples Center jijini Los Angeles, Marekani, ikiwa ni mara ya kwanza kwa msanii huyo kuhudhuria tamasha hilo kubwa.

Hata hivyo, kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo aliweka wazi mwaliko huo na kuwashukuru wote ambao walimuunga mkono kwa mwaka 2016.

“Naamini nafasi hii nimeipata kutokana na kujituma kwangu mwaka 2016 pamoja na mashabiki wangu kuonyesha kunijali, ninawashukuru wote kwa kunijali na kupenda muziki wangu,” alieleza Yemi.
Post a Comment
Powered by Blogger.