Yadaiwa Philippe Coutinho Kuwekewa Uzio Anfiled


Majogoo wa jiji (Liverpool) wamefungua milango ya mazungumzo ya kumsainisha mkataba mpya kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil Philippe Coutinho.

Tovuti ya The Liverpool Echo imeeleza kuwa, Liverpool wamefungua milango ya mazungumzo na kiungo huyo, wakiwa na lengo la kumsainisha mkataba wa muda mrefu.

The Reds wanaamini kipindi hiki ni sahihi kwa Philippe Coutinho kusaini mkataba mpya, kutokana na ushindani unaoendelea kukua siku hadi siku, hususan soko la usajili ambalo linaendelea kufukuta kutoka mashariki na mbali (China).


Mkataba wa sasa wa Coutinho, unatarajiwa kufikia kikomo mwaka 2020, lakini imeanza kuhisiswa huenda mambo yakabadilika wakati wowote, kutokana na kiwango chake kuendelea kuwa tishio kwa klabu nyingine za ndani na nje ya England.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye tayari ameshapachika mabao sita akiwa na kikosi cha Jurgen Klopp tangu mwanzoni mwa msimu huu, anahusishwa na taarifa za kuwaniwa na FC Barcelona, huku tetesi nyingine zikitanabaisha kuwa, klabu za China zinamtolea macho.
Powered by Blogger.