West Ham Yawachomolea Tena Marseille Kumuuza Dimitri PayetWest Ham imekataa ombi jingine la Marseille la kutaka kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Dimitri Payet.

Marseille, wanaocheza Ligue 1, wanaripotiwa kuahidi kutoa pauni milioni moja zaidi ya ombi la hapo awali la pauni milioni 19, lililolkataliwa na mwenyekiti wa West Ham David Sullivan.

Mwenyekiti huyo amesema amechukua uamuzi mkali kwa kukataa kulazimishwa kumuuza mchezaji huyo kwa haraka, huku klabu hiyo ikiwa haina tatizo la kifedha la kutaka kumuuza.

Maneja Slaven Bilic, amesema Payet,29, hataki kuichezea klabu ya West Ham. Payet kwa hivi sasa hafanyi mazoezi na timu ya kwanza na ataendelea kuhudumu na timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23.

Klabu hiyo ya ligi ya Premia imesema ingetaka Payet kuomba msamaha kwa mashabiki na kurudi kujiunga na timu ya kwanza katika mazoezi.
Post a Comment
Powered by Blogger.