Waziri Mkuu Akiri upungufu wa chakula baadhi ya Maeneo


Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu anasema kitendo cha baadhi ya watu kusema Tanzania ina baa la njaa si sahihi kwani kufanya hivyo ni kuwatia hofu wananchi, maana tafsiri ya baa la njaa ni hali kuwa mbaya zaidi, kusema hivyo kutapelekea watu kushindwa kuwa watulivu.

"Tatizo tulilonalo ni katika maeneo yale, mikoa, wilaya ambayo hawakupata mvua kubwa msimu uliopita, utaratibu wetu ni kwamba tunaimarisha masoko ya ndani ili kuhakikisha kwamba maeneo yote yanakuwa na chakula angalau mtu aweze kwenda kununua, kwa hiyo neno baa la njaa ni jambo jingine. Naomba watanzania tusitiane hofu, tusiwatie hofu wananchi kwa kutamka maneno ambayo maana yake halisi kuwa ni hali mbaya zaidi tukafanya watu washindwe kuwa watulivu" alisema Waziri Mkuu 
 
Mbali na hilo Waziri Mkuu amewataka wananchi kuwa wasikivu kwani katika baadhi ya hayo maeneo ambayo kuna upungufu wa chakula serikali imesema inaweza kuwatumia wafanyabiashara wakaleta chakula katika maeneo hayo, pia Waziri Mkuu ameeleza kupanda bei ya chakula katika maeneo mengi ni kutokana na watu wengi kuhifadhi chakula kutokana na hofu ya hali ya hewa ya sasa jambo lililopelekea chakula kupanda bei.
Powered by Blogger.