Wanaigeria Wamjia Juu Mr Eazi Baada Ya Kuudharau Muziki WaoMsanii kutoka Ghana ambae pia ni Mzaliwa wa Nigeria Mr Eazi jana alikuwa kwenye mahojiano na mtandao wa mtandao maarufu wa  Nigeria wa NOTJUSTOK na moja ya vitu ambavyo alivyoongelea ni kuhusu nafasi ya muziki wa Nigeria kwa Bara la Afrika.

Mkali huyo wa Leg Over ambae yupo chini ya Lebo ya Star Boy Music ya Wizkid  alianza kwa kusema Muziki wa Nigeria unapoteza mvuto kwani unahama kila siku kufuata ladha ya muziki wa Ghana ametoa mfano kwa kusema tangia zamani muziki wa Nigeria umekuwa ukikopi staili za muziki wa Ghana kuanzia Beatz mpaka melodi.

Alitolea mfano wa miondoko ya Azonto na Alkaida dance kutoka Ghana ilivyoleta madhara kwenye muziki wa Nigeria mpaka leo bado muziki huo unaendelea kukopi miondoko hiyo,alisema wimbo kama ‘Mad Over u’ wa Run Town ukisikiliza kwa mara ya kwanza unaweza kufikiria ni wimbo kutoka Ghana.

Baada ya Interview hiyo akaona sio mbaya akahamishia maoni yake kwenye ukurasa wake wa Twitter na ndipo akaamsha mashetani ya wanaija kwenye Twitter.

Hizi ni baadhi ya Tweet Hizo

Post a Comment
Powered by Blogger.