Tutegemee Chochote Kutoka Kwa Young Dee N Dogo Janja?

Kama unamfuatilia Dogo Janja basi lazima utakua umekutana na hii ya Mngarenaro Dogo Janja kuonyesha love kwa rapa Young Dee AKA young Daddy anaetamba na ngoma yake "Young Daddy" ambayo ametunga maalum kwa ajili ya mtoto wake wa kike "Tamar"
 Dogo Janja kupitia ukurasa wake wa instagram ametupia picha ya kusapoti ngoma "Young Daady" huku akiiwekea caption ambayo kwa hali ya kawaida ilisomeka kama utani,

  "dogojanjatzSUPPORT #YoungDady LINK KWA BIO YA PAKARAPPER @youngdaresalama "SEMA SIJASKIA UMEWARUSHA SHILAWADU HUMU" maana NDIO WALIOKUFANYA UPATE MWANAO😊"Young Dee nae uvumilivu wa kuikaushia post hiyo hakuweza kuwa nao akajikuta katia neno, Cheki hapo chini alichokijibu Young Dee,"

          " youngdaresalama😂😂 Kwenye remix ile verse yako malizaa."

Tutegemee chochote kufuatia majibu haya ya Young Daresalama kwa Kidebe Master?  Huenda utani huu ukageuka kuwa serious ikiwa haikupangwa hivyo pale miamba hii yenye umri mdogo kwenye game kufuatisha kile ambacho wameshabiki wao wamekichukulia kama deal kwao. Yaani ishu ya kufanyika remix ya ngoma hiyo, 


Hebu fikiria kile ambacho Young Dee amekifanya kwenye Young Daddy halafu vuta pumzi, Ngoja kwanza  mpe Janjaro verse moja kwenye ngoma hiyo?
 Unadhani ngoma hiyo itakua ya aina gani?

 

 IANGALIE HAPA YOUNG DADDY :

Post a Comment
Powered by Blogger.