Tazama Diamond Platnumz Na Rayvanny Walivyotumbuiza Wimbo Wa ‘salome’ Kwenye Tuzo Za CafDiamond Platnumz na Ray Vanny usiku wa Alhamis walifanikiwa kutumbuiza kwa ustadi mkubwa wimbo wa Salome mbele ya watu mashuhuri waliokuwa wamealikwa kuhudhuria tuzo za CAF, Abuja nchini Nigeria.


Tuzo hizo zilikuwa zikiruka live kupitia Supersport 4. Kutumbuiza huko kulikuwa ni hatua kubwa kwa Ray hasa sababu hilo lilikuwa jukwaa kubwa zaidi kwake kutumbuiza tangu aanze muziki.

“Kweli Mungu Akipanga yanatimia,” ameandika kwenye Instagram. “@diamondplatnumz Upendo wako,kujali nakupoteza Muda Wako kwa Ajili ya Vijana wako Hio ndio siri pekee ya safari yako kuwa ndefu zaidi na Mungu Akuongezee Zaidi na zaidi uzidi kwenda mbaaaali.”

“HUA SIAMINI NIKIKUMBUKA NILIKOTOKA NAONA NI NDOTO!!! Sijutii kua Na Uongozi Imara Sana (WCB) @babutale @sallam_sk @mkubwafellatmk @kameboy_j @ricardomomo THANKS ALOT ABUJA NIGERIA AND THE WHOLE #GLOCAFAWARDS CREW,” aliongeza.
Post a Comment
Powered by Blogger.