Tanzia: Aliyekuwa Mwanzilishi Wa Mtandao Wa WorldStarHipHop Afariki Dunia

 Q of WSHH
Mwanzilishi wa mtandao maarufu wa Marekani, WorldStarHipHop, Lee O’Denat aka Q, amefariki dunia usiku wa Jumatatu.

Q aliyekuwa na uzito mkubwa, alikuwa katika harakati za kuupunguza. Amefariki akiwa usingizini. Taarifa zimedai kuwa Q alifariki kutokana na shambulio la moyo, huku unene ukidaiwa kuchangia.

Image result for Lee O’Denat

Watu walio karibu naye wamedai kuwa alikuwa ameanza kwenda gym ili kupunguza uzito kutengeneza muonekano mzuri kwaajili ya show yake mpya ya MTV ambayo ingeanza kuonekana mwaka huu.

Show yake ilikuwa ijumuishe video za kuchekesha pamoja na appearance za mastaa mbalimbali.
Powered by Blogger.