Soulja Boy Afunguka Kinacho endelea Katika Bifu Lake Na Chris Brown


Kwa Bongo kiki ikifanywa na staa yoyote huwa ni kitu cha ajabu sana lakini kumbuka mastaa wakubwa wa Marekani ndio mabingwa wa mambo hayo na wao ndio walioanzisha kwa ajili ya kujiweka juu kila siku.


Wiki hii kumeibuka stori mpya inayohusu bifu kati ya Chris Brown na rapper Soulja Boy huku wakihusishwa kutaka kuzichapa kavu kavu chanzo kilikuwa kikiusishwa kuwa ni mrembo Karrueche Tran.

Soulja Boy ameamua kuweka wazi kila kitu kupitia video aliyopost mitandaoni akidai kuwa hakuna bifu kati yake na Chris ni mipango yao ya kuachia wimbo wao, hiyo imekuja baada ya taarifa za mama yake kukimbizwa hospitalini baada ya kusikia kisanga cha ugomvi huo.


“I just want to send an apology. Over the past couple of months I’ve been acting out, I’ve been wilding out, and at the end of the day it’s not about who starts the beefs, it’s about who ends them. I want to make music with Chris Brown, Yachty, Quavo, everybody,” amesema Soulja kwenye video hiyo.

Naye rapper 50 Cent, kupitia mtandao wa Instagram ameadika, “If we ain’t talking big money, we ain’t talking. Now a whole lot of IG stunting been going on. Where that money at? #wherethebagat.”

Post a Comment
Powered by Blogger.