Soulja Boy Adai Atamdunda Chris Brown Ili Kumlipizia Kisasi Kwa Demu Wake Huyu Wa Zamani Lile pambano la ndondi kati ya Chris Brown na Soulja Boy linazidi kupata promotion zaidi huku kwa upande wake Soulja Boy atanolewa na Floyd Mayweather.

Sasa bad newz nikwamba Soulja Boy amedai kuwa atahakikisha anampa Chris Brown kichapo cha paka mwizi kwenye pambano lao la ndondi ili kumsaidia Rihanna kulipiza kisasi kwa alivyompiga miaka takriban 7 iliyopita.

Kwa mujibu wa rapper huyo, Rihanna alikuwa mtu wake wa karibu enzi ana uhusiano na Chris Brown na kwamba hata alipopigwa alikuwa mtu aliyemliwaza.

Soulja ametumia Twitter kuelezea kufa kwa ushkaji wao na kwamba madawa ya kulevya yamemharibu.

Hizi hapa Tweet za Soulja Boy 

Mbali na hilo pia Tyson amethibitisha kuwa atamnoa Chris Brown. Kuthibitisha hilo amepost video kwenye Instagram na kuandika: It’s official. I’m going to train @chrisbrownofficial. Gonna teach him every dirty trick in the book to knockout @souljaboy. #showup #desertbeatdown #norunning #noexcuses @fredfrenchy

 

 

Post a Comment
Powered by Blogger.