Simba, Azam Haponi Mtu Mapinduzi Cup Usiku Huu

 

Simba na Azam leo zitaumana kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar katika fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kutokana na upinzani uliopo kwa timu hizo zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara. Mara ya mwisho zilikutana kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi mwaka jana na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Simba ilitinga fainali kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-2 na Azam ilifika hatua hiyo kwa kuifunga Taifa Jang’ombe bao 1-0. Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja anadai kuwa ana matumaini makubwa ya kuifunga Azam na kutwaa ubingwa huo.

Alisema walikuwa wakiihofia Yanga na ndio maana walifikishana mpaka kwenye kupigiana penalti lakini kwa Azam hawataki kufikishana huko. Hata hivyo, Mayanja alisema mchezo huo utakuwa mgumu kwani hakuna timu itakayokubali kufungwa kirahisi.

“Azam wanakutana na timu bora baada ya kucheza mchezo uliowashangaza wengi waliposhinda mabao 4-0 dhidi ya Yanga (mechi ya mwisho ya makundi) na sasa tunakutana nao sisi, tutawafunga tu,” alisema.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza Saa 2:15 usiku wa leo, utakuwa ni wa pili kuzikutanisha timu hizo katika fainali ya michuano hiyo
Post a Comment
Powered by Blogger.