Shilole Awachana Wanaolalamika Hali Ngumu


Msanii wa muziki wa bongo fleva Zuhena Mohammed a.k.a Shilole amefunguka na kuwapa neno baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakilalamika juu ya hali ngumu ya maisha huku wengi wao wakiitupia lawama Serikali ya awamu ya tano.

Shilole kupitia mtandao wake wa Instgram amesema amewachana baadhi ya vijana hao na kusema wamekuwa wakilalamika kuwa kuna hali ngumu ya maisha au pesa haipatikani ikiwa wao wenyewe hawahitaji kujishughulisha wamebaki kukaa vijiweni pasipo kuhangaika kutafuta mishe za hapa na pale za kuingiza kipato.

"Unalalamika hali ngumu huku umekaa" aliandika Shilole

Baadhi ya mashabiki wa Shilole wamemuunga mkono kutokana na kauli yake hiyo huku wengine pia wakionyesha kutokubaliana naye wakiendelea kusema kweli maisha ya sasa ni magumu na mishe hakuna.


Post a Comment
Powered by Blogger.