Roma Ataja List Ya Wasanii 5 Wa Hip Hip Bongo Anaowakubali Zidi
Rapa Roma Mkatoliki amefunguka na kutaja orodha ya wasanii wake watano wa hip hop Bongo ambao anawasikiliza na kuwakubali zaidi kutokana na kazi zao.


Roma Mkatoliki kwa kuanza alimtaja Rapa Roho Saba na kusema anamsikiliza sana na kumkubali sana na watu watashangaa kwanini amemtaja Roho Saba ili hali ana ngoma mbili tu ila yeye anasema anazisikiliza sana hizo kazi mbili kuliko kazi nyingine nyingi kutoka kwa wasanii wengine.

 Image result for roma mkatoliki


"Kiukweli nawasikiliza sana wasanii wengi wa Hip hop Bongo lakini kwa kuwa nimepewa nafasi ya kutaja wasanii watano tu wa kwanza nitaanza na mwanangu Jaco Roho Saba, mchizi ana ngoma mbili tu lakini nazisikiliza sana, namkubali sana Jose Mtambo, Prof Jay pia maana kitambo namsikiliza na alini'inspire' toka enzi hizo mpaka leo. Wengine ni Saigoni pamoja na Hashim Dogo" alisema Roma Mkatoliki kwenye Planet Bongo ya EA Radio.

Mbali na hilo pia Roma amedropisha chupa lake Jipya akiwa na Moni Centralzone, Chupa linakwenda kwa jina la "Usimsahau Mchizi". Mpaka sasa chupa hilo linafanya vizuri katika baadhi ya vituo vya Tv mbalimbali nchini.
Post a Comment
Powered by Blogger.