Ripoti: Polisi Kuwashikilia Walio Husika Kumpora Kim Kardashian Ufaransa


Inasemekana kuwa mapolisi wa Ufaransa,Wanafanya juhudi kutafuta majambazi waliomuibia Kim Kardashian vitu vyake vya dhamani mnamo Tarehe 3 mwezi wa kumi,Hotelini Ufaransa.

Kwa mujubu wa chanzo cha habari hii, watu 17 wamekamatwa kama watuhumiwa wa tukio hilo ili kuulizwa maswali, Chanzo hicho kinasema watu 3 wanaosadikiwa kuwa wanawake, walikuwa wakimchunguza Kim siku kabla ya tukio hilo, watuhumiwa 2 wengine wanaaminika kuwa wanajishughulisha na biashara ya Almasi.


Polisi waliweza kuingilia mawasiliano ya watuhumiwa hao kupitia simu walizo zitumia siku ya tukio hilo.

Utawala unasema kuwa msanii huyo raia wa Marekani aliporwa kwa nguvu na takriban watu wawili waliokuwa wamevaa sare za polisi.

Wanaume hao waliingia chumba cha kifahari alichokuwa Kim Kardashiana kabla ya kumfunga na kumfungia kweye bafu. Kisha wanaume hao walitoroka na vito vya thamani ya dola milioni 10.5.

Polisi wa Ufaransa wanasema kuwa uchunguzi wa DNA ndio ulichangia kukamatwa kwa watu hao. Wanaume hao waliakamatwa wakati wa uvamizi ulioendeshwa maeneo ya Paris, Normandy na la Frech Riviera kufutia uchunguzi wa miezi kadha.

Moja ya uchunguzi wa DNA ulikuwa sawa na ule wa mtu anayejulikana kwa polisi kuwa mhalifu. Kardashian ambaye ni mke wa mwanamuziki Kanye West alisema alikuwa na hofu kuwa angeuawa wakati huo.
Post a Comment
Powered by Blogger.