Rapa Ice Boy amekanusha Kufanya muonekano wake kama marehemu 2pac


Rapa Ice Boy ambaye ameachia ngoma yake mpya 'Binadamu' akishirikiana na Nandy amefunguka na kusema yeye haangaiki kutafuta muonekano kama wa marehemu 2 Pac na kusema wala yeye hajifananishi naye ila watu ndiyo wamekuwa wakimwambia anafanana naye

Ice Boy alisema hayo jana kwenye kipindi cha Friday Night Live cha (EATV) na kusema yeye hajifananishi na 2 Pac ila imetokea tu wanafanana na wala yeye hajataka kutumia kiki hiyo katika muziki wake bali yeye anafanya kazi nzuri ambazo watu watazipenda na kumuelewa.

Ice Boy anasema kwa wimbo wake huu mpya amepata baraka zote kwa wasanii wakubwa Tanzania kama Fid Q, Izzo Businness na wengine wengi ambao walimpigia simu na kumpa pongezi kwa kazi nzuri aliyoifanya.


Powered by Blogger.