Quick Rocka: Mwaka 2017 Watu Wategemee Kuniona Nikifanya Collabo Za KimataifaWasanii wengi wa Afrika kwa sasa wamekuwa wakitamani kufanya muziki wao ili ujulikane kimataifa zaidi. Na wengi wao wamekuwa wakitafuta kufanya collabo na wasanii kutoka mataifa mengine. Hii imekuwa ikiwezekana kwa njia hiyo.


Na sasa moja kati ya wasanii ambao wamekuwa wakifanya kazi nzuri, Quick Rocka naye amewaahidi mashabiki wategemee collabo za kimataifa mwaka huu.

“Kila kitu kinaenda na muda na wakati unapofika unakuwa hauna budi kufanya hivyo so nadhani kwa 2017 utakuwa ni muda wangu pia wa kusukuma game yangu mbele zaidi na kutafuta international collabo na vitu kama hivyo, so tuombeane heri tu mambo yaende kama tulivyo panga,” Alisema Quick Rocka.

 Rapper huyo pia ni mmiliki wa studio iitwayo Switch Records iliyofanikiwa kutoa hits kadhaa mwaka jana.
Post a Comment
Powered by Blogger.