Picha: Wakacha Mbioni Kuachia Video Mpya Ya Kundi


Good News kwa mashabiki wa Bongo Flava. Ni kuhusiana na come back ya kundi la Wakacha linalorudi na nguvu mpya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na wasanii wanaounda kundi hilo kuwa kuwa busy na kazi zao binafsi.

Wasanii wanaounda kundi hilo akiwemo Cyril Kamikaze na Jux wameonekana kwenye picha za pamoja ambazo zinawaonyesha wakiwa location wakitengeneza video ya wimbo wao mpya.

Katika kuthibitisha kuwa hiyo ni kazi mpya kutoka kwa kundi hilo, kupitia mtandao wa Twitter Jux ameandika, “WAKACHA we back on it!! @kamikazewakacha.” 

Tazama picha zaidi hapa chini.


   

Mbali na tweet ya Jux pia Rapper Cyril aka Kamikaze, alishawahi kuvujisha siri hiyo wakati akipigia mastori kupitia kipindi cha THE SPLASH kinachosikika kupitia Ebony FM.

“Jana tulikuwa tuko studio mimi, Jux pamoja Flow, tumeshafanya ngoma ,tunachosubiri ni mipango tu ya video. Kwahiyo Wakacha ipo, Wakacha ni familia, Wakacha ni zaidi ya kundi ni kama familia,” alisema Cyril.
Post a Comment
Powered by Blogger.