Picha: Jennifer Lopez Asitisha Ratiba Zake Ili Kuhudhuria Show Ya Drake, Las Vegas

 
Mambo yanazidi kuiva kuhusiana na tetesi za uhusiano kati ya Drake na Jennifer Lopez. Mrembo huyo amelazimika kubadilisha mipango yake yote ya kukaa nyumbani kwa mapumziko ya sikukuu ya mwaka mpya na kwenda Las Veges kumuangalia Drake akitumbuiza.

Vyanzo vya Jennifer Lopez vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa wiki kadhaa zilizopita, muimbaji huyo aliitolea nje ofa kubwa ya kwenda kutumbuiza Miami kwenye mkesha wa mwaka mpya sababu mwaka jana alinunua nyumba mpya na alikuwa akifanya kazi mno kiasi cha kushindwa kuifurahia.0101-jennifer-lopez-watching-drake-perform-nye-new-years-eve-twitter-7 
JLo akiwa katikati ya watazamaji waliohudhuria show ya Drake, Vegas mwishoni mwa wiki.


Alikuwa amepanga kutumia mapumziko ya sikukuu ili kutulia na familia yake. Lakini aliamua kwenda Vegas kutazama show ya Drake, rapper ambaye anadaiwa kuwa na uhusiano naye.

Chini ni picha za Drake akitumbuiza kwenye show hiyo.

A photo posted by champagnepapi (@champagnepapi) on

A photo posted by champagnepapi (@champagnepapi) on

A photo posted by champagnepapi (@champagnepapi) on
Post a Comment
Powered by Blogger.