Nikki wa Pili Astukia Makampuni Yanayoua Muziki Wa Afrika, Afunguka Haya Mazito


Rapa Niki wa Pili ameonesha wasiwasi mkubwa juu ya makampuni makubwa ya muziki ambayo yamekuja kuwekeza Afrika ikiwa pamoja na Afrika Mashariki na kusema lengo kubwa la makampuni hayo ni unyonyaji na kushusha muziki wa Afrika na si kitu kingine.

Nikki wa Pili alisema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, pia alidai wasanii wengi ambao wamesainiwa chini ya kampuni hizo, wengi wao wameshuka kimuziki ukilinganisha na kipindi ambacho walisimama wao kama wao."Afrika Kusini na Nigeria muziki wao wameukuza na kuutangaza wenyewe...toka enzi za P Square mpaka Wizkid, au toka Marium Makeba mpaka Mafikizolo. ujio wa wageni ndiyo unakuja kuushusha. Mtazame Davido toka amesainiwa na Sony na kabla ya hapo...au Keko wa Uganda, au Rose Mhando..hawa walisainiwa Sony...na pili makampuni hayo lengo ni kufungua milango ya huku kwa muziki wa nje...ndiyo maana Mtv Awards main artist alikuwa Future" alisema Nikki wa Pili 
Post a Comment
Powered by Blogger.