Nikki wa Pili Adai Mashabiki Wamekacha Shoo


Rapa anayefanya poa katika Muziki wa Hip Hop Bongo, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ amekiri mashabiki wengi kuacha kujitokeza katika shoo mbalimbali nchini kutokana na uchumi kuyumba.

Akizungumza na Showbiz, Nikki wa Pili anayebamba na Ngoma ya Sweet Mangi alisema, amekuwa akisikia kuyumba kwa uchumi na wasanii wengi wa Bongo Fleva wamekuwa wakitegemea kupata hela kupitia shoo lakini kwa hali ya sasa ilivyo imekuwa ngumu.


“Kwa sasa huwezi kukuta mashabiki wanajitokeza kwa wingi kwenye burudani kama zamani kwa sababu mfukoni hawana kitu. Mashabiki wengi bajeti zao wamezielekeza kwenye mahitaji muhimu tu, burudani wameiweka kando kwa muda, maana yake ni kwamba kazi ya muziki tunapolekea itakuwa mbaya,” alisema Nikki.
Post a Comment
Powered by Blogger.