Nay wa Mitego: Ukitaka Shindana Na Mimi Jiandae Kufilisika, Karibu Mjengoni Free Nation Records


Kupitia akaunti ya Instagram ya Nay wa Mitego ameshare picha ambazo zinaonyesha kukamilika kwa studio yake iliyoleta mzozo baada ya  kuitangaza studio hiyo kama zawadi kwa Producer wake kwa kumfanyia bits nzuri za nyimbo.

Kutokana na ugomvi uliosemekana kutokea miezi sita iliyopita Nay wa Mitego ndipo alipoamua kuichukua studio na kuihamisha ilipokuwa mwanzo na kuipeleka sehemu nyingine.


Studio hiyo kwa sasa tayari inaonekana imeshaanza kufanya kazi katika eneo iliyohamishiwa. Moja kati ya caption ambazo zipo kwenye video hiyo, Nay ameandika.. "#’FreeNationRecords2017Mchakamchaka’ #PumziUnayo.?! Mungu ni Mwema. mabaya yao Mungu anageuza Kheri kwangu . Ukitaka kushindana namimi jiandae kufirisika Karibuni mjengoni  #FreeNationRec. Palipo Barikiwa kutoa Mziki wenye hela, GoodMusic. #MoneyMusic‘".
Powered by Blogger.