Nay Wa Mitego Anyoosha Maelezo Kilevi Anachotumia


Nay wa Mitego ni msanii ambae misimamo yake ya kuwapa watu makavu hususani ma-star wenzake au hata watu maarufu kwenye tasnia nyingine huwa haoni tabu kivile kwani hakuna mtu asiyemjua kwa hilo.

Sasa leo kupitia kipindi cha Klabu 101 cha Capital Radio Nay wa Mitego aliulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho, kuwa anatumia Bangi au kilevi chochote?Nay alisikika akijibu kuwa kwa sasa hatumii kilevi chochote kile bali amesema miaka 16 iliyopita alikuwa mtumiaji mzuri wa vitu hivyo.

Niliwahi kuvuta Bangi ila ni zamani sana kama miaka 16 hivi iliyopita lakini kwa sasa situmii kilevi chochote kile sio bangi,sio pombe wala sigara,Mimi kilevi changu ni familia yangu kwani ni kilevi tosha“Alisema Mr Nay.

Mbali na hilo, hivi sasa rapa huyo yupo katika vita nzito ya vijembe vya maneno kwenye interview pamoja na mtandaoni na msanii mwezake kutoka Manzese, Madee.
Post a Comment
Powered by Blogger.