Nay Wa Mitego Adai Mwaka Huu Atafanya Collabo Zaidi Na Wasanii Wa Kike


Mwaka 2017 ni mwaka ambao wasanii wetu wa Bongo Flava wameahidi kufanya vizuri ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuendana na ushindani uliopo kwa sasa kwenye Music Industry.

Kama ilivyokuwa miaka mingine,mwaka huu pia tutashuhudia collabo nyingi za ndani na nje ya nchi ambazo wasani wetu watazifanya kama walivyoahidi. Lakini rapper Nay Wa Mitego yeye hafikirii kuwapa kipaumbele wasanii wa kiume kwenye collabo atakazozifanya kwa mwaka huu.Nay anadai kuwa, kuna collabo atazifanya mwaka huu, lakini zaidi atafanya na wasanii wa kike “Nafikiria kufanya collabo zaidi na wasanii wa kike, ndio wasanii ambao nafikiria nadhani watafaa zaidi kwenye nyimbo zangu,” amesema Nay.

Mkali huyo wa Hip hop Bongo anafanya vizuri na mgoma yake ya Sijiwezi aliyoiachia mwishoni mwa mwaka jana.
Post a Comment
Powered by Blogger.