Navy Kenzo Wadai Ilikuwa Ni Moja Ya Mpango Wao Kuachia AlbumWasanii Aika na Nahreel ambao wanaunda kundi na Navy Kenzo wamefunguka na kusema kuwa album yao ya 'AIM' itawapa thamani zaidi kama wasanii hata kama haitaweza kurudisha au kuwapa pesa za kutosha lakini itawaongezea thamani kama wasanii. 


Navy Kenzo walidai kuwa huo ulikuwa ni moja ya mpango na kwamba wao waliona hawawezi kuendelea na 'career' yao kama wasanii ikiwa watakuwa hawana album.


 "Sisi tunaona ni muhimu msanii kuwa na album hata kama hutapata pesa lakini ni muhimu kwanza inakupa thamani kama msanii, tuliona Navy Kenzo hatuwezi kuendelea na career yetu bila kuwa na album, hivyo tunajivunia. Huenda inaweza isiingize kitu sana ila itatuongeza thamani zaidi. Maana hata tunapokwenda kwa wenzetu huko unaona kabisaa msanii bila album anakuwa hana thamani kivile" alisema Nahreel kwenye EA Radio

Mbali hilo Aika alisisitiza kuwa waliona umuhimu wa album yao ndiyo maana waliamua kuipa heshima kwa kufanya kazi kubwa nzuri ambazo nyiingine wameshiriakiana na wasanii wakubwa.

"Sisi Alikiba tunamuona ni mtu mwenye kipaji kikubwa uwepo wake kwenye album yetu unaleta baraka kubwa, na si Alikiba tu wapo wengine wasanii wakubwa wengine kama  Patoranking, R 2 Bees, Mr Eazi hivyo nadhani sisi tunaheshimu kazi ya sanaa lakini tuliiheshimu sana album yetu ndiyo maana tuliipa nguvu kama hivi" alisisitiza Aika
Post a Comment
Powered by Blogger.