Navy Kenzo Wabadili Ratiba Ya Rama Dee, Rama Dee Afunguka


Kundi la Navy Kenzo ambalo tayari limeachia mtaani albam yake ya Above In A Minute (AIM) limemfanya msanii mkali wa R&b Tanzania Rama Dee kubadili tarehe ya utoaji wa albam yake.

Rama Dee baada ya kusikiliza albam ya Navy Kenzo alitoa mawazo yake kuwa ni kati ya albam bora ambayo imepikwa vyema na ipo kwenye ubora wa hali ya juu na kuwataka watu kuitafuta albam hiyo na kusikiliza.


"Baada ya kusikiliza hii album nimebadilisha tarehe ya utoaji wa albam yangu! Albam hii ni kali sana Nahreel you did my friend, Good on you, please nenda nunua hii albam ni nzuri sana ipo kwenye kiwango kizuri kabisa haina ujanja ujanja" aliandika Rama Dee kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Post a Comment
Powered by Blogger.