Mr T Touch Atoa Povu Hili Kwa Nay Wa Mitego Kwa Kutumia Beat ya 'Sijiwezi' Bila Makubaliano Naye, Msikie Hapa


Mtayarishaji wa zamani wa studio ya Nay wa Mitego ‘Free Nation’ Mr T Touch amefunguka na kuzungumzia hujuma na aliyekuwa bosi wake baada ya wawili hao kudaiwa kuachana vibaya na Nay wa Mitego kutumia Beat bila idhini ya Mr T.

13736136_1027734437295098_733240745_n

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm Alhamisi hii, Mr T Touch amesema alishamchana Nay kutotumia hatimiliki yake, lakini Nay akaifanyia kibabe labda kutokana na studio ilikuwa yake.

"Nikamwambia bwana hii beat nahitaji kutumia kivingine kwa sababu haiwezi kukaa studio, hii beat ni nzuri, ndio mimi nikampa Black Rhyino", alisema T 

Aliendelea, "Ila kwa sababu Nay documents alikuwa nazo pale studio, akaichukua hii (sijiwezi) akaifanyia kibabe kwa sababu ile studio ilikuwa yake, jambo ambalo mimi sijalipenda ndo maana nilisema 'Usitumie hatimiliki' yangu." 

Aliongeza, "kwa sababu hiyo nyimbo (sijiwezi) eti kafanya na maproducer wa nne? kitu ambacho sio kweli, hii beat yote ni yangu mimi".

Hii hapa full Interview, unaweza kusikiliza mengi aliyofunguka Mr T


Post a Comment
Powered by Blogger.