Mourinho Adai Martial Anafaa Kunisikiliza Mimi Sio Ajenti Wake

Anthony Martial kushoto na mkufunzi Jose Mourinho


Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Anthony Martial anafaa kunisikiza mimi na sio ajenti wake ,mkufunzi wa kilabu hiyo Jose Mourinho amesema.

Ajenti wa raia huyo wa Ufaransa ameripotiwa akisema kuwa anaangalia chaguo la mteja wake kwenda kuchezea Sevilla.

Martial mwenye umri wa miaka 21 alikuwa mchezaji mwenye mabao mengi katika klabu ya United msimu uliopita akiwa na mabao 17 ,lakini bao lake la kusawazisha siku ya Jumamosi lililosaidia United kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Middlesborough ni la tano msimu huu.

''Ni mchezaji ambaye anaweza kuwa maarufu sana'' ,alisema Mourinho. ''Martial alicheza ,alisaidia na kufunga.Alipigania mipira,alikuwa na lengo na najua ni talanta kubwa''.


 Anthony Martial akifunga bao la kusawazisha dhidi ya Boro siku ya Jumamosi

Martial ambaye alijiunga na The Red Devils kutoka Monaco kwa pauni milioni 36 mwaka 2015 alikuwa kiungo muhimu baada ya timu yake kutoka nyuma na kuilaza.

Alifunga bao kunako dakika ya 85 kabla ya Paul Pogba kufunga bao la ushindi kwa kichwa dakika moja baadaye.
Post a Comment
Powered by Blogger.