Huku Ukiwa Unasubiri Video Ya Ay Na Nyanshiski, Enjoy Na Hii Mistari Yao


Upepo wa Industry ya game ya muziki wa bongo unazidi kuwa mtamu, Magoma kibao yanazidi kuachiwa kila kukicha, Kitu kizuri zaidi hakuna ngoma inayotoka na ikabuma kwa wakati huu, Yaani kila ngoma inayotoka ni kitu juu ya kitu.

Mzee Wa Commercial @Aytanzania ni mmoja kati ya wanamuziki ambao wanaenda sawa na upepo huo, Ngoma yake "More N More" aliyoshirikiana na Mkenya Nyanshiski imo miongoni mwa zile ngoma zinazosikilizwa sana wiki hii.
.

Tunamtambua AY kwenye list ya wabongo wanaopzitendea haki ngoma zao kwa kuzitengenezea vichupa vikali,

 Ukiachana El Chapo ambayo ndio Video yake ya mwisho "Zigo Remix" ambayo alifanya na @Diamondplatnumz ndio video yake inayoongozwa kwa kuangaliwa kwenye mtandao wa YouTube, Mpaka time hii Video ya "Zigo Remizx" imetazamwa zaidi ya mara milioni nane.(8,338,09)

ANGALIA ZIGO REMIX YA AY FT. DIAMOND PLATNUMZ:Macho ya mashabiki na wadau wa muziki wa AY lazima yatakua yameelekezwa kwenye ujio wa Video ya ngoma "More & More" ambayo mpaka sasa bado haijaachiwa licha ya Audio ya ngoma hiyo kuendelea kufanya vizuri.

 Kabla Ya Video Ya Ngoma "MoreNMore" Rapa Ay amewazawadia mashabiki wake video yenye mashairi ya ngoma hiyo. 

ENJOY NA MISTARI YA AY NA NYANSHISKI HAPA: DOWNLOAD HAPA AUDIO YA NGOMA HIYO"
Powered by Blogger.