Mohd Faiz Ashinda Tuzo Ya Mfungaji Wa Bao Bora Zaidi Wa Mwaka


Mchezaji kandanda kutoka Malaysia Mohd Faiz Subri ameshinda Tuzo ya Puskas inayotolewa na FIFA kwa mfungaji wa bao bora zaidi wa mwaka.

Faiz, anayechezea klabu ya Penang FA ndiye raia wa kwanza kabisa wa Malaysia kuwa mshindi wa tuzo hiyo.

Mohd Faiz Subri

Mchezaji huyo wa miaka 29 kutoka Penang alipata karibu asilimia 60 ya kura zilizopigwa kwa bao lake la frikiki alilofunga mechi ya Ligi Kuu ya Maaysia dhidi ya timu ya Pahang mwezi Februari.

Alikabidhiwa tuzo hiyo na mchezaji soka mahiri kutoka Brazil, Ronaldo.

Ronaldo

Waliokuwa wanashindania tuzo hiyo mwaka huu ni Marlone na kiungo wa kati wa Venezuela Daniuska Rodriguez.

Cristiano Ronaldo wa Ureno na Real Madrid alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani na kumshinda Lionel Messi wa Barcelona na Argentina.
Post a Comment
Powered by Blogger.