Michuano Mikali kati ya wababe Azam FC na Simba FC nani Ataibuka kidedea?

Kwa mara ya mwisho Simba na Azam Fc walikutana katika michuano ya Kombe la Mapinduzi ambao Simba walifungwa bao 1-0 katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar na kuwafanya Azam Fc kufanikiwa kutwaa kombe la Mapinduzi kwa mara ya 3.

Kwa ushindi huo wa Azam FC ulikuwa sawa na kulipa kisasi cha kipigo kama hicho cha 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Septemba 17, mwaka jana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa bao pekee la Shiza Kichuya.

Baada ya kila timu kushinda mechi moja katika michezo miwili iliyozikutanisha timu hizo msimu huu, leo zinakutana kwa mara ya tatu na ya mwisho katika msimu huu.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuchezeshwa na refa Erick Onoka atakayesaidiwa na washika vibendera Hassan Zani, wote wa Arusha na Josephat Masija wa Mwanza, wakati mezani atakuwapo Soud Lila wa Dar es Salaam na Kamisaa ni Michael Bundala.

Mchezo wa leo ni muhimu zaidi kwa Simba kushinda, wao ndiyo wapo kwenye mbio za ubingwa wakifukuziwa kwa karibu mno na mahasimu wao wa jadi, Yanga SC.

Simba SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 45 ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 43 baada ya kila timu kucheza mechi 19.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wameonyesha wasiwasi juu ya mchezo huu huku wengine wakiombea timu yao iweze kufanya vizuri huku wengine wakiomba hata droo katika mchezo huu. 
Powered by Blogger.