Mfahamu Melody Mbassa: Msanii Mpya Wa Kumwangalia Kwa Mwaka 2017


Kila mwaka wasanii wapya hujitokeza kujaribu bahati zao kwenye muziki. Si wote wanaoweza kufanikiwa na kwa wengine wenye vipaji halisi kama Melody Mbassa hufika mbali.


Melody Mbassa si msanii mchanga kama wengi wanavyofahamu, alianza kuimba miaka ya 2003 na kusikika rasmi kwenye vipindi vya watoto na hit single ya "Toto Party". Kwa sasa Melody ameingia kwenye muziki rasmi na ameonekana kupokelewa vizuri juu ya muziki anaofanya.

Kama utausikiliza wimbo wake ‘Nikukoleze’ utakubali bila ubishi kuwa muziki ni kipaji chake na wala halazimishi. Hakika ni mmoja wa wasanii wapya wa kuwaangalia sana mwaka 2017.

Hii hapa kazi yake inayofanya vizuri kwa sasa "Nikukoleze" ambayo imepata matokeo chanya mara baada ya kuachiwa kwake.


Powered by Blogger.